Al-Mu´taqad as-Swahiyh Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas
Yüklə 0.94 Mb.
səhifə6/7
tarix26.04.2016
ölçüsü0.94 Mb.
1   2   3   4   5   6   7

7. ´Aqiydah sahihi juu ya muislamu mtenda dhambiAhl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuwa hakuna dhambi, mbali na shirki, inayomtoa muislamu katika Uislamu isipokuwa pale atapoihalalisha. Ni mamoja akawa ni mwenye kuifanya na huku anaona kuwa ni halali au akawa anaamini kuwa ni halali pasi na kuifanya. Kwa sababu hii ina maana ya kwamba atakuwa ni mwenye kuikadhibisha Qur-aan na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo ni kufuru kwa mujibu wa Kitabu, Sunnah na maafikiano.

Hakuna dhambi inayomfanya mwenye nayo kudumu Motoni milele isipokuwa tu shirki. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

"Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae." (04:48)

Aayah imefahamisha kuwa mtenda dhambi yuko chini ya matakwa ya Allaah; Akitaka (Ta´ala) kumsamehe atamsamehe kwa fadhila na ukarimu Wake, na Akitaka atamuingiza Motoni kwa kiasi cha dhambi yake ili umsafishe na madhambi halafu baada ya hapo atamtoa kutokana na Tawhiyd yake kisha amwingize Peponi.

Allaah ametaja baadhi ya madhambi makubwa katika Kitabu Chake. Baadhi yake ni kuua na manyanyaso. Hata hivyo Amethibitisha imani kwa wenye nayo. Mtu kama huyo ni muumini kwa imani yake, mtenda dhambi kwa dhambi zake. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ"Enyi mlioamini! Mmeandikiwa shariy’ah kisasi waliouawa. Muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa wema." (02:178)

Amemthibitishia (Ta´ala) imani yule muuaji na muuliwaji kama ambavyo amethibitisha kuwa ni wandugu katika imani. Hakuna mgongano wa kutumia neno "dhambi" katika kitendo au yule mtendaji, kumwita yule mtendaji muislamu na kumpitishia zile hukumu za Kiislamu juu yake. Kitu kinachoweka hilo wazi, ni kile kisa cha ´Abdullaah bin Himaar ambaye alikuwa anakunywa pombe. Pindi alipoletwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Swahabah mmoja akasema:

"Allaah akulaani. Ni wingi uliyoje unaletwa!"

Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:"Usimlaani; hakika anampenda Allaah na Mtume Wake."

Dhambi hii haikumtoa katika Uislamu. Bali uhakika wa mambo ni kuwa alimthibitishia imani, pamoja na kutumbukia katika dhambi hii kubwa. Kitu kinachobainisha hilo, ni kuwa kufuru, shirki, dhuluma, dhambi na unafiki vimegawanyika aina mbili katika Shari´ah:

Aina kubwa: Aina hii ni ile inayomtoa mtu katika Uislamu.

Aina ndogo: Aina hii inapingana na ukamilifu wa imani wa yule mwenye nayo pasi na kumtoa katika Uislamu.

Mgawanyiko huu umebainishwa na Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Mmoja katika wabingwa wa Ummah na mfasiri wa Qur-aan, Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), amesema kuwa kuna kufuru ndogo, dhuluma ndogo, dhambi ndogo na unafiki mdogo. Allaah amemwita yule mwenye kuomba badala Yake kwamba ni "kafiri", "mshirikina" na "dhalimu". Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ"Na yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake - hakika hawafaulu makafiri." (23:117)

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا"Sema: “Hakika mimi namuomba Mola wangu Pekee na wala simshirikishi na yeyote."" (72:20)

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ

Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa na wala asiyekudhuru. Endapo utafanya hivo, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu." (10:106)

إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ"Isipokuwa Ibliys alikuwa miongoni mwa majini akaasi amri ya Mola wake." (18:50)

Haya yote yanahusiana na kufuru kubwa, shirki kubwa, dhuluma kubwa na dhambi kubwa ambavyo haviwezi kukusanyika na imani. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

"Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri." (05:44)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ"Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu." (05:45)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ"Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki." (05:47)

إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا"Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto na watauingia [Moto wa] Sa’iyraa." (04:10)

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):"Kumtukana muislamu ni dhambi na kumpiga vita ni kufuru."

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):"Mwenye kuapa kwa mwengine asiyekuwa Allaah amekufuru au ameshirikisha."

Haya yanahusiana na kufuru ndogo, shirki ndogo, dhuluma ndogo na dhambi ndogo ambavyo vinaweza kukusanyika na imani, kama ilivyokuja katika Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Mambo haya yanafanya imani kupungua na kupingana na ukamilifu wake.


08. ´Aqiydah sahihi juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuwapenda Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kujenga urafiki nao, kuwatakia radhi na kuwaombea msamaha na kuwasifia. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ"Na wale waliotangulia awali miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia mabustani yapitayo chini yake mito - ni wenye kudumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa." (09:100)

Allaah (Ta´ala) amewaridhia waliotangulia awali pasi na kushurutisha wema. Kuhusu wale waliokuja nyuma, hayuko radhi na wao endapo hawatowafuata kwa wema. Amesema (Ta´ala):

لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ

"Kwa yakini Allaah Amewawia radhi waumini walipofungamana nawe ahadi ya utiifu chini ya mti." (48:18)

Yule ambaye Allaah ameridhika naye basi hatomkasirikia maishani. Imethibiti katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:"Hakuna yeyote aliyetoa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti atayeingia Motoni."

Allaah amewaelezea Muhaajiruun na kuwasifu ya kwamba ni wakweli. Amesema (Ta´ala):

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ

"Kwa ajili ya mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na [zikataifishwa] mali zao wanatafuta fadhila na Radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake - hao ndio wakweli." (59:08)

Halafu Akawataja Answaar na kusema:

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

"Na wale waliokuwa na makazi na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohajiri kwao na wala hawapati kuhisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wameshikwa na ufukara. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu." (59:09)

Kisha Akataja (Ta´ala) hali za waumini baada yao wenye kuwafuata Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa wema na kusema:

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

"Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini. Mola wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu." (59:10)

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا"Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na Radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat na mfano wao katika Injiyl kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake liwapendezeshe wakulima ili kuwakasirisha makafiri. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao msamaha na ujira mkubwa." (48:29)

Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

"Yule ambaye moyoni mwake mna chuki dhidi ya mmoja katika Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi anaingia ndani ya Aayah:

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالَّذِينَ آوَوا وَّنَصَرُوا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ"Na wale walioamini na wakahajiri na wakafanya jihaad katika njia ya Allaah na wale waliotoa makazi na wakanusuru - hao ndio waumini wa kweli. Watapata msamaha na riziki tukufu." (08:74)

Amesema (Ta´ala) juu ya Maswahabah akibainisha fadhila za wale waliojitolea na kupigana kabla ya Ushindi - mkataba wa Hudaybiyah - juu ya wale waliojitolea na kupigana baada ya Ushindi - lakini makundi yote mawili yameahidiwa Pepo na Allaah:

لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

"Na mna nini hata hamtoi katika njia ya Allaah na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allaah Pekee. Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baada [ya ushindi] na wakapigana - na wote Allaah Amewaahidi Pepo. Na Allaah kwa yote myatendayo ni Mjuzi." (57:10)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Msiwatukane Maswahabah zangu."

Katika matamshi ya Muslim imekuja:"Msimtukane yeyote katika Maswahabah zangu. Lau atakuwepo mtu atayetoa dhahabu mfano wa [mlima wa] Uhud, basi hautofikia Mudd wala nusu ya mmoja wao."

Mudd ni robo ya Swaa´ [chini ya gramu mia sita] na nusu yake ni nusu ya Mudd.

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa ´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Watu bora ni karne yangu, kisha wataofuatia, kisha wataofuatia." ´Imraan amesema: "Sijui alisema karne mbili au tatu baada ya karne yake." Halafu baada ya hapo watakuja watu wataotoa ushuhuda pasi na kuombwa kushuhudia, watafanya khiyana pasi na kuaminiwa, wataweka nadhiri pasi na kutimiza na kutadhahiri kwao kuipenda dunia."

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya Answaar:"Alama ya imani ni kuwapenda Answaar. Alama ya unafiki ni kuwachukia Answaar."

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa al-Baraa´ bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu Answaar:"Hakuna anayewapenda isipokuwa muumini tu na hakuna anayewachukia isipokuwa mnafiki tu. Allaah anampenda yule mwenye kuwapenda na Allaah anamchukia yule mwenye kuwachukia."

Muslim amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:"Hakuna mtu anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho anayewachukia Answaar."

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu kisa cha Haatwib bin Abiy Balt´ah:"Ameshuhudia [vita vya] Badr. Allaah aliwatazama watu wa Badr na kusema: "Fanyeni mtakalo, hakika Nimekusameheni.""

Muslim amepokea kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema kuwa Umm Mubashshir alimsimulia ya kwamba alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema kwa Hafswah:"Hakuna yeyote katika wale waliokula kiapo cha usikivu na utiifu atayeingia Motoni - Allaah akitaka."

Walikuwa watu zaidi ya 1400 na miongoni mwao alikuwa Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy.

Ahl-us-Sunnah wanaitakidi kuwa mbora wa Ummah huu baada ya Manabii wake ni Abu Bakr as-Swiddiyq. Kisha ´Umar al-Faaruq. Haya ni kwa maafikiano ya Maswahabah na Taabi´uun. Hakuna yeyote katika wao aliyepingana na hili.

Kumepokelewa mapokezi tele kutoka kwa kiongozi wa Waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba amesema:"Wabora wa Ummah huu baada ya Manabii wake ni Abu Bakr na ´Umar."

Ahl-us-Sunnah wanaonelea kuwa watatu ni ´Uthmaan na wanne ni ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhumaa).


1   2   3   4   5   6   7


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©azrefs.org 2016
rəhbərliyinə müraciət

    Ana səhifə