Al-Mu´taqad as-Swahiyh Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas
Yüklə 0.94 Mb.
səhifə5/7
tarix26.04.2016
ölçüsü0.94 Mb.
1   2   3   4   5   6   7

05. ´Aqiydah sahihi juu ya imaniKatika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni pamona na kuonelea kuwa imani ni kutamka shahaadah ya upwekeshaji ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kuyaamini yakini maneno haya na matendo ya viungo vya mwili. Imaam ash-Shaafi´iy amesema:

"Maswahabah, Taabi´uun na wale tuliokutana nao walikuwa ni wenye kuafikiana kwa kusema kwamba imani ni maneno, matendo na nia. Mtu halipwi kwa kuacha moja katika hivyo vitatu."

Imepokelewa na al-Laalakaa´iy katika "as-Sunnah".

Imani inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi. Allaah (Ta´ala) amesema:

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا

"Wale walioambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni" yakawazidishia imani." (03:173)

وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ"Wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea." (08:02)

وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ"Na inapoteremshwa Suurah, basi miongoni mwao wako wanaosema: “Nani kati yenu [Suurah] hii imemzidishia imani? Ama wale walioamini huwazidishia imani nao wanafurahia." (09:124)

وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا"Basi waumini walipoona yale makundi, walisema: “Haya ndio yale Aliyotuahidi Allaah na Mtume Wake na Amesema kweli Allaah na Mtume Wake - na haikuwazidishia isipokuwa imani na kujisalimisha." (33:22)

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ"Yeye Ndiye Aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za waumini ili Awazidishie imani pamoja na imani zao." (48:04)

وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا"Na iwazidishie imani wale walioamini." (74:31)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Ibn ´Umar ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatolea mawaidha wanawake na akawaambia:"Sijaona walio na akili punguani na dini pungufu wanaomghalibu mtu mwenye busara kama nyinyi [wanawake]."

Hii ni dalili juu ya kupungua kwa imani. Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):"Muumini aliye na imani kamilifu zaidi ni yule aliye na tabia njema zaidi."

Ameipokea Ahmad na wengineo kutoka kwa Abu Hurayrah.

Ikiwa ambaye yuko imani kamilifu zaidi ana tabia njema zaidi, basi aliye na tabia mbaya ana imani pungufu zaidi.

Imani sio maneno na matendo peke yake pasi na kuamini, kwa kuwa hii ni imani ya wanafiki. Amesema (Ta´ala):

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ

"Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho" hali ya kuwa si wenye kuamini."" (02:08)

Wala imani sio kule kuwa na utambuzi peke yake, kwa kuwa hii ni imani ya makafiri na wakanamungu. Amesema (Ta´ala):

وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا

"Wakazikanusha na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha kwa dhulma na majivuno." (27:14)

فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ"Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha Aayaat za Allaah." (06:33)

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ"Wale Tuliowapa Kitabu wanatambua kama wanavyotambua watoto wao." (02:146)

وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ"Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao na japokuwa hapo kabla walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru, basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah iwe juu ya makafiri." (02:89)

وَعَادًا وَثَمُودَ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَاكِنِهِمْ ۖ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَكَانُوا مُسْتَبْصِرِينَ"Na [Tuliwaangamiza pia kina] ‘Aad na Thamuud na yamekwishakubainikieni masikani yao; na shaytwaan aliwapambia ‘amali zao akawazuia na njia, na walikuwa ni wenye kumaizi." (29:38)

Kadhalika imani sio maneno na kuamini pasi na matendo. Allaah ameyaita matendo kuwa ni imani. Amesema (Ta´ala):

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ"Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza imani zenu." (02:143)

Bi maana swalah zenu kuelekea Yerusalemu. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kuuambia msafara wa ´Abdul-Qays:"Ninakuamrisheni mambo mane; kumuamini Allaah na hivi mnajua ni nini kumuamini Allaah? Ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kutoa khumusi ya mateka yenu."

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea vilevile kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:"Imani ni tanzu sabini na kitu - au ni tanzu sitini na kitu. Bora yake ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na ya chini yake ni kuondosha chenye kudhuru njiani na hayaa pia ni tanzu katika imani."

06. Msimamo wa Ahl-us-Sunnah juu ya TakfiyrHakuna kitendo chochote kukiacha kwake ni kufuru isipokuwa swalah peke yake. Yule mwenye kuiacha pasi na kifungamanishi basi amekufuru. Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameafikiana juu ya hilo. ´Abdullaah bin Shaqiyq amesema:

"Hakuna kitu Maswahabah wa Mtume wa Allaah ambacho walikuwa wakionelea kukiacha kwake ni kufuru isipokuwa swalah."

Ameipokea at-Tirmidhiy.

Takfiyr ni haki ya Allaah. Asiwepo atayemkufurisha yeyote isipokuwa tu yule ambaye amekufurishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au mtu ambaye waislamu wameafikiana juu ya kumkufurisha.

Ambaye atamkufurisha mtu kwa kitu kisichokuwa ukafiri ambacho kimesimama juu ya hoja zilizo wazi kutoka katika Qur-aan tukufu, Sunnah Swahiyh au maafikiano, basi mtu huyo anastahiki adhabu kali na kuaziriwa. Kwa sababu al-Bukhaariy amepokea kupitia kwa Thaabit bin adh-Dhwahhaak (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Mwenye kumtuhumu muumini ukafiri basi ni kama kumuua."

Kufuru inaweza kupatikana kwa kutamka neno, kufanya kitendo na kuitakidi imani fulani ya kufuru ambayo hakuna tofauti yoyote inayozingatiwa. Miongoni mwa mambo vilevile yanayoshurutisha ukafiri ni mtu kuhalalisha [kitu au jambo la haramu].

Tofauti kati ya kukufurisha kwa jumla na kumkufurisha mtu maalum: kukufurisha kwa jumla ni kama makemeo ya jumla. Mtu anatakiwa kusema vile ilivyo kama ambavyo haikufungamana na kwa ujumla wake. Mfano wa hilo ni kama walivyosema maimamu:

"Mwenye kusema Qur-aan imeumbwa ni kafiri."

Ibn Khuzaymah (Rahimahu Allaah) amesema:

"Ambaye hathibitishi kuwa Allaah amelingana juu ya ´Arshi na yuko juu ya mbingu saba ni kafiri ambaye damu yake ni halali. Mali yake inakuwa fai."

Kuhusu kumkufurisha mtu maalum ni lazima masharti yatimie na kusiwepo vikwazo. Kukufurisha kwa jumla ambako hakufungamana hakupelekei kumkufurisha mtu maalum mpaka yatimie masharti ya kukufurisha na vikwazo viondoke.

1   2   3   4   5   6   7


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©azrefs.org 2016
rəhbərliyinə müraciət

    Ana səhifə