Al-Mu´taqad as-Swahiyh Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas
Yüklə 0.94 Mb.
səhifə1/7
tarix26.04.2016
ölçüsü0.94 Mb.
  1   2   3   4   5   6   7

al-Mu´taqad as-Swahiyh Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas
المعتقد الصحيح
الواجب على كل مسلم اعتقاده

al-Mu´taqad as-Swahiyh

[I´tiqaad sahihi wajibu kwa kila Muislamu kuiamini]

Mwandishi:

Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym

Tarjama:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush


00. Dibaji ya kitabu al-Mu´taqad as-Swahiyh
4

01. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah


9

02. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat


13

03. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah


16

04. ´Aqiydah sahihi juu ya nguzo za imani sita


23

05. ´Aqiydah sahihi juu ya imani


47

06. Msimamo wa Ahl-us-Sunnah juu ya Takfiyr


51

7. ´Aqiydah sahihi juu ya muislamu mtenda dhambi


53

08. ´Aqiydah sahihi juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)


56

09. ´Aqiydah sahihi juu ya watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)


61

10. ´Aqiydah sahihi juu ya karama za mawalii


63

11. ´Aqiydah sahihi juu ya watawala wa waislamu


65

12. Msimamo sahihi juu ya mijadala katika dini


67

13. Matahadharisho ya kukaa na Ahl-ul-Ahwaa´


69

14. Hitimisho ya kitabu


70


00. Dibaji ya kitabu al-Mu´taqad as-SwahiyhHimdi zote anastahiki Allaah. Swalah na salaam ziwe juu ya Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake.

Amma ba´d:

Hakika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ndio dini ya haki ambayo ni wajibu kwa kila muislamu aiitakidi, kwani ndio ´Aqiydah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake watukufu (Radhiya Allaahu ´anhum). Atakayechagua ´Aqiydah nyingine, basi ameipelekea nafsi yake katika adhabu, khasira na ghadhabu za Allaah kali.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu mapote ambayo yatazuka katika Ummah wake na akataja mapote sabini na tatu:"Yote yatakuwa Motoni isipokuwa moja tu ambalo ni al-Jamaa´ah."1

Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesifu mkusanyiko huu ambao umesalimika kutokamana na matishio ya Moto pale aliposema:"Ni wale wataokuwemo katika mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah."2

Hiki ndio kidhibiti cha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hakika wao ni wenye kushikamana na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Sunnah za makhaliyfah wake waongofu. Ni wenye kuziuma kwa magego. Kwa ajili hio ndio maana wakawa ni pote lililookoka (Firqat-un-Naajiyah). Ni wenye kuokoka na Moto siku ya Qiyaamah. Ni wenye kusalimika na Bid´ah hapa duniani. Vilevile wao ni kundi lililonusuriwa (Firqat-ul-Mansuurah). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:"Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu kuwepo katika haki wazi wazi mpaka itapowajia amri ya Allaah ilihali wako wazi wazi."

"Hakutoacha kuwepo kipote kwenye Ummah wangu katika ushindi mpaka itapowajia amri ya Allaah ilihali ni washindi."3

Maana ya kuwa wazi hapa ni nusura (Ta´ala):

فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ

"Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi." (61:149)

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ"Na hakika jeshi Letu ndilo litakaloshinda." (37:173)

Wao ni wenye kushinda kwa panga na mikuki au kwa hoja na dalili. Inahusu kundi moja na sio mengi. Kwa ajili hiyo ndio maana wameitwa ´mkusanyiko`. Amesema (Ta´ala):

فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ

"Na kuna nini baada ya haki ila upotofu." (10:32)

Hawatambuliki kwa jina lingine zaidi ya Uislamu na Sunnah na majina mengine yenye dalili. Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

"Ahl-us-Sunnah hawana jina lingine wanalotambulika kwalo, si Jahmiyyah, Qadariyyah wala Raafidhwah."

Aliulizwa vilevile kuhusu as-Sunnah ambapo akajibu kwa kusema:

"Hawana jina lingine zaidi ya as-Sunnah."

Bi maana Ahl-us-Sunnah hawana jina wanalojinasibisha nalo zaidi yalo.

Kumetiliwa umuhimu mkubwa juu ya kuipa nguvu ´Aqiydah ya wema waliotangulia (Salaf-us-Swaalih) na kubainishwa dalili zake. Imewekwa wazi na maimamu wengi wakubwa katika vitabu vingi, vya kibinafsi na vya kwa pamoja. Miongoni mwa vitabu hivyo kuna vinavyoitwa "as-Sunnah", bi maana "´Aqiydah". Ni zaidi ya vitabu mia mbili na khamsini. Baadhi yavyo ni:

1 – ”as-Sunnah” ya Ibn Abiy ´Aaswim

2 – ”as-Sunnah” ya ´Abdullaah bin Imaam Ahmad

3 – ”as-Sunnah” ya al-Khallaal

4 – ”as-Sunnah” ya Ahmad bin al-Furaat Abiy Mas´uud ar-Raaziy

5 – ”as-Sunnah” ya Ismaa´iyl bin Usayd al-Madiyniy

6 – ”as-Sunnah” ya Ibn-ul-Qaasim – mwanafunzi wa Maalik

7 – ”as-Sunnah” ya Muhammad bin Salaam al-Baykandiy

8 – ”as-Swifaat wa ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah” ya Nu´aym bin Hammaad

9 – ”as-Sunnah” ya al-Athram

10 – ”as-Sunnah” ya Harb bin Ismaa´iyl al-Karmaaniy

11 – ”as-Sunnah” ya Ibn Abiy Haatim

12 – ”as-Sunnah” ya Ibn Jariyr at-Twabariy

13 – ”at-Tabasswur fiy ´Alam-id-Diyn” vilevile ni ya Ibn Jariyr

14 – ”as-Sunnah” ya at-Twabaraaniy

15 – ”as-Sunnah” ya Abush-Shaykh al-Aswbahaaniy

16 – ”as-Sunnah” ya Abul-Qaasim al-Laalakaa’iy

17 – ”as-Sunnah” ya Muhammad bin Naswr al-Marwaziy

18 – ”´Aqiydat-us-Salaf wa Asw-haab-il-Hadiyth” ya as-Swaabuuniy

19 – ”al-Ibaanah” ya Ibn Battwah

20 – ”at–Tawhiyd” ya Ibn Khuzaymah

21 – ”at-Tawhiyd” ya Ibn Manda

22 – ”al-Iymaan” ya Ibn Abiy Shaybah

23 – ”al-Iymaan” ya Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Salaam

24 – ”Sharh-us-Sunnah” ya al-Muzaniy – mwanafunzi wa ash-Shaafi´iy

25 – ”Sharh-us-Sunnah” ya al-Baghawiy

26 – ”Sharh Madhaahib Ahl-is-Sunnah” ya Ibn Shaahiyn

27 – ”al-Hujjah fiy Bayaan-il-Mahajjah wa Sharh ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah” ya Abul-Qaasim al-Aswbahaaniy

28 – ”Usuul-us-Sunnah” ya Abu Abdullaah Ibn Abiy Zamaniyn

29 – ”ash-Shariy´ah” ya al-Aajurriy

30 – ”I´tiqaad Ahl-is-Sunnah” ya Abu Bakr al-Ismaa´iyliy

31 – ”as-Sunnah” ya al-Barbahaariy

32 – ”al-Iymaan” ya Ibn Manda

33 – ”al-Iymaan” ya al-´Adaniy

34 – ”al-´Arsh” ya Ibn Abiy Shaybah

35 – ”al-Qadar” ya Ibn Wahb

36 – ”al-Qadar” ya Abu Daawuud

37 – ”ar-Ru’yah” ya ad-Daaraqutwniy

38 – ”as-Swifaat” ya ad-Daaraqutwniy

39 – ”an-Nuzuul” ya ad-Daaraqutwniy

40 – ”Jawaab Ahl Dimashq fiys-Swifaat” ya al-Khatwiyb al-Baghdaadiy… na vitabu vinginevyo vingi.

Vivyo hivyo inahusiana na vitabu vilivyoandikwa baada ya waandishi hawa. Miongoni mwao ni Ibn ´Abdil-Barr, Ibn Qudaamah al-Maqdisiy, Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, adh-Dhahabiy, Ibn Kathiyr, Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na wengineo. Humo mmebainishwa ´Aqiydah sahihi. Vinasimamisha hoja na kufichua utata wa Ahl-ul-Ahwaa´.

Tutataja sehemu katika ´Aqiydah ya watu hawa vigogo.

Sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Allaah. Kwake Yeye ninategemea na kwake Yeye naelekea.

  1   2   3   4   5   6   7


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©azrefs.org 2016
rəhbərliyinə müraciət

    Ana səhifə